Vyombo vya habari vya China na
wananchi wamelalamikia kiasi kikubwa cha uchafuzi wa hewa katika mji
wa kusini wa Shenyang, ambao wanaharakati wamesema ni mchafuzi mbaya
kuwahi kutokea katika nchi hiyo.
Hadi siku ya jumapili kiwango cha
kipimo uchafuzi wa hewa kilionyesha alama mara 50 juu, ya kiwango cha
uchafuzi wa hewa kinachochukuliwa kuwa ni salama na Shirika la Afya
Duniani.
Chombo cha habari cha umma
kimeishutumu serikali ya mji huo kwa kuachilia hali hiyo ya kuwepo
kwa moshi mzito.
Uchafuzi wa hali ya hewa ni tatizo
sugu kaskazini mashariki mwa China, ambako kunaviwanda vingi vya
makaa ya mawe.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni