Ikulu ya Kenya imeendelea kuwa kimya
iwapo rais Uhuru Kenyatta atahudhuria sherehe za kuapishwa rais
mteule Dk. John Pombe Magufuli licha ya taarifa ya serikali ya
Tanzania kusibitisha ujio wake.
Mkurugenzi Mwandamizi wa Mawasiliano
ya Ikulu ya KenyaBw. Munyori Buku alipoulizwa na vyombo vya habari
vya nchi hiyo jana kuhusu rais Kenyatta kuhudhuria sherehe hizo
hakuthibitisha wala kukanusha suala hilo.
Taarifa ya serikali ya Tanzania
imesema rais Kenyatta ataungana na viongozi Robert Mugabe wa
Zimbabwe, Yoweri Museveni wa Uganda, Paul Kagame wa Rwanda, Jacob
Zuma wa Afrika Kusini, Joseph Kabila wa (DRC), Filipe Nyusi wa
Msumbiji pamoja na Edgar Lungu wa Zambia.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni