.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 13 Novemba 2015

KAIMU MKURUGENZI MUHIMBILI AKUTANA NA BARAZA LA WAFANYAKAZI

1
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Mseru akifafanua jambo katika mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa hospitali hiyo leo. Kushoto ni Katibu wa Baraza hilo, Clive Leonard Urima na kulia ni Katibu msaidizi, Domiana John.
2
Mwakilishi wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE), Fortunatus Chuwa akichangia mada kwenye mkutano wa Baraza la Wafanyakazi ambao umefanyika leo jijini Dar es Salaam.
3
Mmoja wa wafanyakazi wa hospitali hiyo, Cresensia Joseph John akichangia mada kwenye mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
4
Katibu wa Chama Cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE), Gaudensi Kadyango akiwasilisha mada kwenye mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH). Mkutano huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam.
678
Baadhi ya wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Lawrence Mseru kwenye mkutano wa Baraza la Wafanyakazi.

PICHA ZOTE KWA HISANI YA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI (MNH)

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Mseru leo amekutana na Baraza la Wafanyakazi la Hospitali hii katika kikao cha 15 cha Baraza hili.
 

Katika kikao hicho wafanyakazi wamezungumzia changamoto zinazoikabili MNH na mafaniko mbalimbali yaliopatikana yakiwamo uboreshaji wa miundo mbinu na upatikanaji wa huduma kwa kiwango cha juu.
 

Profesa Mseru amewataka Wakurugenzi, Wakuu wa Idara pamoja na Mameneja wa Majengo kusimamia vizuri wafanyakazi wa MNH watimize wajibu wao ili kuongeza tija mahali pa kazi.
 

“Kila mmoja anapaswa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria na mkataba wake wa kazi ili kufikia malengo,”amesema Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Mseru.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni