Nchi ya Kenya nayo imeonekana
kufuata nyayo za Tanzania za kupiga marufuku safari za nje, baada ya
serikali ya nchi hiyo nayo kutangaza kusitisha safari zote za nje za
watumishi wa umma nchini humo.
Agizo hilo limetolewa Waziri wa
Fedha, Henry Rotich, ili kuokoa fedha za serikali ambapo katika mwaka
wa fedha ulioisha maafisa wa umma walitumia shilingi bilioni 20 za
Kenya kwa safari, ambazo ni sawa na karibu nusu ya bajeti ya afya.
Katika matumizi hayo ya safari za
nje na za ndani serikali kuu ilitumia shilingi za Kenya bilioni 10.8
na serikali za kaunti zilitumia shilingi bilioni 9.2 za nchi hiyo.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni