Wanawake wawili waliojilipua kwa
mabomo ya kujitoa mhanga wameuwa watu 11 katika soko la mji mkuu wa
kaskazini wa Kano nchini Nigeria.
Wakazi wa eneo hilo wamesema mabomu
hayo yalilipuka ndani ya soko la simu za mkononi, na lingine katika
mlango wa kuingilia soko hilo.
Hakuna kundi lililodai kuhusika na
tukio hilo lakini wapiganaji wa kundi la Boko Haram wamekuwa
wakihusika katika mashambulizi yaliyotokea mji wa Kano.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni