Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani
Papa Francis amesema milango ya makanisa ya kikatoliki duniani
inapaswa kuwa wazi licha ya hofu ya usalama baada ya mashambulizi ya
Jijini Paris.
Akiongea na mahujaji St Peter square
nchini Italia Papa Francis ameyataka makanisa Katoliki duniani
kutoweka ulinzi mkali milango, kwani milango ya kanisa inapaswa kuwa
wazi kwa watu.
Amesema kuwa kunamaeneo duniani
ambayo milango inapaswa kufungwa kwa funguo, na kuna baadhi ya maeneo
milango hulindwa kwa ulinzi mkali na hilo limeanza kuwa ni kama
desturi.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni