Kiongozi wa mashambulizi ya Jijini
Paris, Abdelhamid Abaaoud, ametambuliwa kuwa ni miongoni mwa
waliouwawa na polisi katika msako kwenye kitongoji cha Saint Denis.
Mwendesha mashtaka amesema mwili wa
Abaaoud ulikutwa ukiwa na risasi pamoja na matundu mengine ya mlipuko
katika chumba kilichoshambuliwa kwa risasi na polisi.
Abdelhamid Abaaoud, 28, mwenye uraia
wa Ubelgiji alitambuliwa kutokana na alama zake za vidoleni.
Mashambulizi ya Ijumaa Jijini Paris
yanayohusishwa na kundi la Dola ya Kiislam (IS) yaliuwa watu 129 na
mamia kujeruhiwa.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni