Na:George Binagi-GB Pazzo wa Binagi Media Group
Mwanahabari Nashon Kenedy kutoka gazeti la
kiswahili la Habari Leo na lile la kiingereza la Daily News amewashauri
wasanii wa maigizo Jijini Mwanza, kubadilika na kuigiza filamu
zinazogusa maisha halisi ya Kitanzania na kuachana na uigizaji wa filamu
zisizo na uhalisia wa maisha ya Kitanzania hususani filamu za
mapenzi.
Kenedy aliyasema hayo jana katika hafla ya
kuzaliwa kwa Yusuph Kisiba a.k.a Yuskiss ambae ni Mtengenezaji wa
Filamu katika Kampuni ya Shafineyz Film Production ya Jijini Mwanza
ambapo alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo ambayo pamoja na wageni
wengine, pia ilihudhuriwa na wasanii mbalimbali wa muziki na filamu
kutoka Jijini Mwanza.
Japokuwa maisha yetu yanategemea mapenzi,
lakini mimi nawashauri kwamba acheni kuigiza filamu za mapenzi kila
siku kama mnahitaji kufanikiwa. Igizeni filamu zinazoeleza maisha halisi
ya kitanzania kama vile kuonyesha matatizo yanayowakabili wananchi, na
hapo ndipo mtaweza kuwa tofauti na waigizaji wengine jambo ambalo
litawasaidia kufikia katika mafanikio yenu". Alibainisha
Kenedy.
Katika hafla hiyo, Kisiba aliwashukuru
wale wote walioungana nae katika kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa
ambapo aliahidi kuitimiza ahadi yake ya kuhakikisha kuwa soko la
uigizaji wa filamu Jijini Mwanza linafufuliwa kupitia Kampuni
anayofanyia kazi ya Shafineyz Film Production kwa kuwa ni aibu
kukosekana kwa soko la filamu Jijini hapa ikilinganishwa na majiji
mengine nchini kama vile Jiji la Dar es salaam.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni