.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 22 Novemba 2015

KENYA YAPELEKA JESHI MPAKANI NA ETHIOPIA BAADA YA POLISI WAKE KUUWAWA

Wanajeshi wa Kenya na maafisa polisi wamepelekwa katika mpaka wa Kenya na Ethiopia eneo la Sololo, katika Kaunti ya Marsabit baada ya kuuwawa maafisa polisi watatu wa Kenya na wanajeshi wa Ethiopia siku ya Ijumaa.

Wanajeshi wa Ethiopia waliingia katika mipaka ya Kenya na kuwauwa kwa kuwapiga risasi maafisa polisi watatu wa Kenya, kuharibu gari la polisi na kisha kuchukua silaha nne huko Anona, Kaunti ya Marsabit.

Kamishna wa kaunti ya Marsabit Moffat Kangi amesema wanajeshi pamoja na polisi wapo tayari wakilinda usalama katika maeneo ya Ramole na Anona katika mpaka wa Kenya na Ethiopia, ambapo tayari miili ya maafisa wa polisi waliouwawa imesafirishwa kwa ndege Nairobi.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni