Michuano ya Kombe la Shirikisho ya Azam Sports inafunguliwa rasmi Jumapili (Novemba 8, 2015) kwa mechi tatu zitakazochezwa kwenye viwanja vitatu tofauti.
Mechi rasmi ya ufunguzi itakuwa kati ya wenyeji JKT Rwamkoma ya Mara na Villa Squad ya Dar es Salaam itakayofanyika kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma.
Siku hiyo pia kutakuwa na mechi kati ya Kariakoo ya Lindi na Changanyikeni FC ya Dar es Salaam itakayochezwa kwenye Uwanja wa Ilulu mjini Lindi, wakati Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Wenda FC ya Mbeya na Madini SC ya Arusha.
Bingwa wa michuano hiyo inayodhaminiwa na Azam Sports HD ataiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika mwaka 2017.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni