Miili ya watu 144 waliokufa siku ya
jumamosi katika ajali ya ndege nchini Misri, imesafirishwa kurejeshwa
St Petersburg Urusi wakati uchunguzi wa chanzo cha ajali hiyo
ukiendelea.
Watu wote 224 waliokuwa kwenye ndege
hiyo wengi wao wakiwa raia wa Urusi wamekufa baada ya ndege hiyo
kuanguka kaskazini mwa penisula ya Sinai.
Taifa la Urusi liliitumia siku ya
jana kufanya maombolezo ya kitaifa baada ya ajali hiyo mbaya ya
ndege.
Polisi wa Urusi wakisubiri kupokea miili ya watu 144



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni