Watu
wasiofahamika wanatafutwa na jeshi la polisi mkoani Kagera, kutokana
na kusababisha vifo vya watu wanne waliokatwakatwa mapanga na miili
yao kufunikwa na majani ya migomba.
Mauaji
hayo yalitokea usiku wa kuamkia leo katika kijiji Ilogelo kata Katoma
wilaya ya Bukoba, baada ya watu wasiojulikana awali kuwavamia watu
wawili na kuwaua kwa kuwafyeka kwa mapanga kabla ya kufanya mauaji
kama hayo kwa watu wengine wawili katika kata hiyo.
Kamanda
wa polisi mkoani Kagera, Augustini Ollomi, aliwataja waliouawa katika
matukio hayo ni Kaijage John (30), Anastella Paschal (42), Emmanuel
Joseph (30) na Evodius Alloyce ambaye umri wake haujatambulika wote
wakiwa wa kijiji cha Illogelo.
Kamanda
Ollomi alisema, awali wauaji hao walianza kutekeleza mauaji yao kwa
watu wawili (Kaijage John na Anastella Paschal), ambao walikumbwa na
umauti huo wakati wakitoka matembezini na kurejea nyumbani.
Watu
wasiofahamika wanatafutwa na jeshi la polisi mkoani Kagera, kutokana
na kusababisha vifo vya watu wanne waliokatwakatwa mapanga na miili
yao kufunikwa na majani ya migomba.
Mauaji
hayo yalitokea usiku wa kuamkia leo katika kijiji Ilogelo kata Katoma
wilaya ya Bukoba, baada ya watu wasiojulikana awali kuwavamia watu
wawili na kuwaua kwa kuwafyeka kwa mapanga kabla ya kufanya mauaji
kama hayo kwa watu wengine wawili katika kata hiyo.
Kamanda
wa polisi mkoani Kagera, Augustini Ollomi, aliwataja waliouawa katika
matukio hayo ni Kaijage John (30), Anastella Paschal (42), Emmanuel
Joseph (30) na Evodius Alloyce ambaye umri wake haujatambulika wote
wakiwa wa kijiji cha Illogelo.
Ollomi
alisema, awali wauaji hao walianza kutekeleza mauaji yao kwa watu
wawili (Kaijage John na Anastella Paschal), ambao walikumbwa na
umauti huo wakati wakitoka matembezini na kurejea nyumbani.
Alisema
mara baada ya wauaji hao kutekeleza unyama huo, waliifunika miili ya
marehemu hao kwa kutumia majani ya migomba kisha kwenda kufanya
mauaji kama hayo kwa (Joseph na Alloyce) na kuwafunika kutumia majani
hayo ya mgomba.
Kutokana
na mauaji hayo ya kinyama, jeshi la polisi linaendesha msako wa
kuwatafuta wauaji hao huku likiomba msaada kutoka kwa raia wema,
viongozi wa dini na wa serikali ili kutoa taarifa sahihi zisizo na
nia ya kuoneana juu ya wahusika waliotenda unyama huo kwa lengo la
sheria kufuata mkondo wake.
Hata
hivyo, Ollomi alisema wahusika wa mauaji hao si wageni katika mkoa
huo, hivyo kuwaomba wananchi kushirikiana vizuri na polisi na muda si
mrefu wanaweza kupatikana ili hatua za kishera zichukue mkondo wake.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni