Mlipuko katika Mji wa Yola nchini
Nigeria umesababisha vifo vya watu kadhaa na kuwajeruhi wengine, huku
baadhi ya taarifa zikisema zaidi ya watu 30 wanaweza kuwa wamekufa.
Mlipuko huo umetokea katika eneo la
soko lenye harakati nyingi, ambapo wakati ukitokea wafanyabiashara
walikuwa wakijianda kufunga soko.
Rais wa Nigerian, Muhammadu Buhari
ametembelea Yola silu ya jumamosi, na kutangaza kuwa wapiganaji wa
kundi la Kiislam la Boko Haram wapo karibu kudhibitiwa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni