.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 18 Novemba 2015

NYOTA WA HOLLYWOOD CHARLIE SHEEN AKIRI KUISHI NA VIRUSI VYA HIV

Nyota wa Hollywood Charlie Sheen amethibitisha kuwa anamaambukizi ya virusi vya Ukimwi, katika mahojiano yaliyofanywa na kituo kimoja cha runinga nchini Marekani.

Sheen ambaye amekuwa akitambulika sana kwa ukorofi, matatizo ya ulevi na matumizi ya dawa za kulevya amekiri kuwa yeye anaishi na virusi vya HIV.

Nyota huyo wa tamthilia ya Two And A Half Men amejitokeza katika shoo ya NBC's Today, na kukiri kupata maambukizo ya ugonjwa huo na kumaliza uvumi uliodumu kwa muda mrefu.

Sheen amesema wakati alipowaambia marafiki zake kuwa ameambukizwa virusi hivyo, baadhi walianza kumtishia kutoboa siri na kulazimika kuwalipa fedha ili kuwaziba mdomo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni