Duh, leo inanyesha kweli. Mkuu wa mkoa wa Kilimnajaro, Amos Makalla ( kushoto ) akiwa amejikinga na mvua alipowasili hifadhi ya Taifa ya mlima Kilimanjaro (KINAPA)
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Amos Makalla ametembelea Hifadhi ya Taifa ya
mlima Kilimanjaro (KINAPA) na kufanya kikao na menejimenti ya Kinapa,
kukagua njia wanazopita watalii, utaratibu wa kuwapokea na kuwapandisha
watalii mlima Kilimanjaro.
Ameipongeza Kinapa kwa kuwa miongoni mwa hifadhi 5 zinazojiendesha
vizuri na kuchangia mapato ya serikali, kuchangia ajira zaidi ya watu 100,000
kwa mwaka na usimamamizi madhubuti wa sheria za uhifadhi wa mazingira
na kuanza kurejesha hali ya theluji ya mlima kilimanjaro iliyoanza
kupungua kwa muda mrefu.
Katika ziara hiyo ameiagiza menejimenti kufanya yafuatayo:-
1. Kusimamia kwa nguvu zote eneo la hifadhi lisiingiliwe na shughuli za kilimo, ujangili man uharibifu wa vyanzo vya maji.
2. Kufanya mikutano na vijiji vyote 80 vinavyozunguka hifadhi kwa lengo
la kuelimisha umma faida na hasara zitakazopatikana baada kuharibu
mazingira.
3.Kuwafungia na kuwanyanganya leseni makampuni yanayopandisha watalii
yanayotuhumiwa kwa udanganyifu , utapeli unaopelekea watalii kukosa
huduma na kutapeliwa.
Aidha amewataka wananchi wa mkoa kilimanjaro kuendelea kupanda miti na kulinda mlima kilimanjaro na vyanzo vya maji
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni