Ulinzi ukiwa umeimarishwa nje ya uwanja wa Wembley nchini Uingereza kabla ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki utakaochezwa leo usiku katika uwanja huo baina ya wenyeji Uingereza dhidi ya Ufaransa.
Mchezo huo unachezwa zikiwa ni siku nne tu zimepita tangu mashambulio ya kigaidi yafanyike jijini Paris nchini Ufaransa ambapo jumla ya watu 129 waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa.
Kikosi cha timu ya taifa cha Ufaransa kilisafiri kwenda London kuwavaa England katika mchezo huo wa kirafiki usiku wa leo baada ya kukataa kuahirisha kutokana na mashambulio ya kigaidi yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Paris.
Kikosi cha timu ya soka cha Ufaransa kikiwasili mapema leo asubuhi katika uwanja wa Wembley jijini London
Ulinzi ukiwa umeimarishwa ndani ya uwanja wa Wembeley jijini London
Ulinzi ukiwa umeimarishwa nje ya uwanja wa Wembley jijini London nchini Uingereza.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni