Mshambuliaji Jamie Vardy amevunja
rekodi aliyoweka Ruud van Nistelrooy, baada ya jana kuwa mchezaji wa
kwanza kufunga magoli 11 mfululizo katika mechi za Ligi Kuu ya
Uingereza.
Mshambuliaji huyo wa Leicester
alifunga goli katika kipindi cha kwanza katika mchezo ulioishia kwa
sare ya bao 1-1 dhidi ya Manchester United.
Mholanzi Van Nistelrooy aliweka
rekodi ya kupachika mabao 10 mfululizo akiwa na Manchester United
katika msimu wa 2003.
Goli hilo la Vardy linafanya idadi
ya mabao 14 aliyoyafunga katika msimu huu na kuongoza kwa kupachika
mabao hadi sasa.
Bastian Schweinsteiger akifunga pao lake kwa kichwa


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni