Watu wapatao 40 wamekufa na makumi
kujeruhiwa huku mamia wakiwachwa bila ya makazi kufuatia mvua kubwa
zinanzonyesha nchini Kenya.
Hapo jana mtoto wa kiume amepoteza
maisha baada ya kuzama kwenye maji katika machimbo ya kokoto Taita
Taveta ambapo alikuwa akicheza na rafiki zake.
Mvua kubwa zimeathiri karibu nusu ya
nchi ya Kenya katika kaunti 24, huku Shirika la Msalaba Mwekundu
likiongoza jitihada za kuokoa waathirika wa mafuriko.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni