Nyota wa Hollywood Jean-Claude Van
Damme ametinga katika mazoezi ya timu ya Manchester City na kupata
muda wa kupiga picha na wachezaji wa timu hiyo wakiwemo Wabelgiji
wenzake Vincent Kompany na Kevin De Bruyne.
Nyoto huyo anayetambulika kama mtu
mwenye misuli kutoka Ubelgiji, alitengeneza jina lake katika filamu
kama Bloodsport, Hard Target na Universal Soldier, yupo Jijini
Manchester kuhudhuria hafla black-tie dinner.
Mbabe huyo mkongwe wa mapigano ya
kickboxer ambaye kwa sasa amekuwa akioneakana mno kwenye matangazo ya
bia kuliko kwenye filamu pia alipiga picha na wachezaji Yaya Toure,
Sergio Aguero pamoja na kocha Manuel Pellegrini.
Van Damme akiwa na Vincent Kompany
Van Damme akiwa na Sergio Aguero
Van Damme akiwa na kocha wa Man City Manuel Pellegrini
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni