Chama Tawala cha Burundi kimewataka
raia wote wa Ubelgiji ambao ni taifa lililokuwa likiitawala nchi hiyo
wakati wa ukoloni, waondoke nchini humo.
Nchi ya Burundi inaituhumu Ubelgiji,
kujihusisha na makundi ya upinzani ambayo inawashutumu kwa wimbi la
mauaji.
Machafuko ya Burundi yalianza Aprili
mwaka huu wakati rais Pierre Nkurunziza alipotangaza dhamira yake ya
kuwania urais kwa muhula wa tatu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni