.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 20 Novemba 2015

WAPIGANAJI WA KIISLAM WATEKA WATU HOTELINI NA KUUWA WATU WATATU


Wapiganaji wa Jihadi wenye silaha wamewauwa watu wapatao watatu katika tukio la mashambulizi ya silaha na kuteka wengine 170 katika hoteli ya Radisson Blu huko Bamako, nchini Mali.

Milio ya risasi imesikika kwenye ghorofa ya saba ya hoteli hiyo yenye vyumba 190, ambapo inasadikiwa wapiganaji 10 wamekuwa wakipita kila ghorofa na kuwateka wageni 140 na wafanyakazi 30.

Mashahidi wamesema kuwa wapiganaji hao wenye silaha wamewaruhusu watu 20 kutoka katika hoteli hiyo baada ya kujiridhisha kuwa ni waislam kufuatia kusoma aya za Kuraan mbele ya wapiganaji hao.
                Wanajeshi wakiwa na silaha huku watu waliofanikiwa kutoka hotelini wakikimbia

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni