.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 10 Novemba 2015

POLISI AFYATUA RISASI NA KUUWA WAMAREKANI WAWILI NCHINI JORDAN

Askari polisi mmoja amefyatua risasi katika kituo cha mafunzo nchini Jordan na kuwauwa Wamarekani wawili, Muafrika Kusini mmoja na wa Jordan wawili.

Ubalozi wa Jordan Jijini Washington, umesema polisi huyo pia amewajeruhi Wamarekani wawili na wa Jordan wawili kabla na yeye kuuwawa kwa kupigwa risasi.

Rais Barack Obama amesema Marekani inachukulia shambulizi hilo kwa umakini.

Kituo hicho cha Mafunzo ya Polisi kinachofadhiliwa na Marekani nchini Jordan kinatoa mafunzo kwa maafisa polisi wa nchi za Palestina na Irak.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni