Vyama vya upinzani nchini Afrika
Kusini vimeshinikiza serikali kuachana na mipango ya kununua ndege ya
rais Jacob Zuma ambayo itagharimu dola milioni 280.
Wizara ya Ulinzi imeweka tangazo la
kutaka kununua ndege hiyo yenye chumba cha kulala pamoja na chumba
cha mikutano.
Ikulu ya Afrika Kusini, imeitaka
idara inayohusika na manunuzi ya ndege hiyo kuuarifu umma kuhusiana
na manunuzi ya ndege hiyo.
Hata hivyo Katibu wa Wizara ya
Ulinzi ya Afrika Kusini Bw. Sam Gulube ameviambia vyombo vya habari
hajui gharama ya ndege hiyo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni