Rais wa Taiwan Ma Ying-jeou
atakutana na rais wa China Xi Jinping Jijini Singapore jumamosi ikiwa
ni kwa mara ya kwanza kufanya hivyo kwa marais wa mataifa hayo.
Mazungumzo hayo ya pande hizo mbili
yatajikita katika kuboresha uhusiano na Taiwan.
China ilidai kuwa kisiwa cha Taiwan
ni dola lake tangu mwaka1949, baada ya serikali ya kitaifa kukimbia
baada ya kudhibitiwa na Wakomonisti.
Hata hivyo uhusiano umeimarika tangu
rais Ma aingie madarakani mwaka 2008.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni