Klabu ya Soka ya Real Madrid ya
nchini Hispania imekutana na kipigo cha kwanza katika ligi ya La Liga
msimu huu cha mabao 3-2 kutoka kwa Sevilla katika mchezo wa Ligi Kuu
ya Hispania uliopigwa jana usiku.
Wakiwa ugenini Madrid walianza
kupata bao lililofungwa na Sergio Ramos lakini Sevilla wakafunga
mabao matatu kupitia Cillo Immobile, Ever Banega na Fernando
Lloriente huku bao la pili kwa Real Madrid likifungwa na James
Rodrigues.
Kipigo hicho kwa Madrid kinaiacha
Barcelona kutamba kileleni kwa pointi 27, pointi tatu mbele ya Real
Madrid baada ya jana vijana wa Jose Henrique kuibuka na ushindi wa
nabao 3-0 jana usiku dhidi ya Villarreal.
Sergio Ramos akisikilizia maumivu ya bega baada ya kufunga bao kwa mtindo Bicycle Kick.
Neymar akifurahia bao alilofunga
Luis Suarez akifurahia bao la penati alilofunga




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni