Rais wa Baraza Kuu la 70 la Umoja wa Mataifa, Bw. Mogens Lykketoft akizungumza kabla ya kumpa nafasi Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon, wakati Baraza hilo lilipokutana pamoja na mambo mengine kujadili ajenda ya uboreshwaji wa utendaji kazi wa Ofisi ya Rais wa Baraza Kuu. Majadiliano hayo yalitawaliwa na tuhuma nzito za rushwa zinazomkabili aliyekuwa Rais wa Baraza Kuu la 68 la Umoja wa Mataifa. Bw. John Ashe. Akizungumzia tuhuma hizo, Ban Ki Moon amesema vitendo vya rushwa haviwezi kuvumiliwa ndani ya chombo hicho na kwamba tuhuma hizo zimeathiri taswira na heshima ya Umoja wa Mataifa.
Na MwandishiMaalum, New York
Tuhuma za rushwa zinazoambatana na ukwepaji kodi zinazomkabili aliyekuwa Rais wa Baraza Kuu la 68 la Umoja wa Mataifa, Bw. John Ashe ,siyotu, zimeitingisha Moja ya Taasisi Kubwa duniani katika nyanja ya Diplomasia na Ushirikiano wa kimataifa, bali pia kunaifanya Taasisi hiyo kujipima na kujipanga upya.
Tuhuma nzito zinazomkabili Rais huyo wa Baraza Kuu la 68 ziliibuka kwa mara ya kwanza tarehe sita mwezi Octoba mwaka huu, baada ya vyombo vya habari vya hapa Marekani kukutaarifu zilizotolewa na Serikali ya Marekani kwamba, imemkamata Bw. Ashe kwa tuhuma za kupokea rushwa na ukwepaji wa kodi kutoka kampuni moja ya Kichina, wakati akiwa Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Katika siku nzima ya Juzi (Jumanne) Baraza Kuu la 70 la Umoja wa Mataifa ambalo lipo chini ya Urais wa Bw. Mogens Lykketoft lilikutana kwa majadiliano ya ajenda kadhaa ikiwa moja ya uboreshaji wa mfumo wa utendaji kazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Katika mkutano huo ambao pia ulihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Ban ki Moon , suala la Bw. John Ashe ambaye kwa sasa yupo nje kwa dhamana.
Akizugumza wakati wa majadiliano hayo. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye ameonyesha wazi kukerwa na tuhuma hizo tangu zilipoibuka, amesema heshima na hadhi ya Umoja wa Mataifa umomashakani kutokana na tuhuma hizo.
Akawaeleza Wajumbe wa Baraza hilo kuwa Umoja wa Mataifa unatakiwa kujifunza kupitia tuhuma hizo huku akisisitiza kuwa hapatakuwa na msamaha kwa yeyote atakayehusika na rushwa katika Umoja wa Mataifa.
Akabainisha kwamba tayari ameiagiza Ofisi za Ukaguzi wa Ndani za Umoja wa Mataifa, kuanza uchunguzi na ukaguzi kwa ushirikiano kati ya UM, Mfuko wa Malengo ya Maendeleo Endelevu na Kampuni ya Kian Ip Group kuangalia matumizi ya fedha zilizopokelewa kutoka taasisi hizo.
Bw. John Ashe ambaye alihudumu kama Rais wa Baraza Kuu la 68 tangu mwezi Septemba 2013 hadi Septemba 2014 alikamatwa pamoja na watu wengine watano kwa tuhuma za rushwa za mabilioni ya dola.
Katika hotuba yake, Ban Ki Moon amesema kutokana na majukumu makubwa na mengi yanayolikabili Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa,ambalo linachukuliwa kama Bunge la Kimataifa, nchi wanachama wa UM wanaowajibu wakuboresha na kuimarisha utendaji wa Baraza hilo kwa kulipatia raslimali fedha na watendaji wenyewe Uledi.
Kwa upande wake, Rais wa Baraza Kuu la 70 Bw. Moges Lykketoft akizungumza wakati wa majadiliano hayo, alitangaza kuundwa kwa kanuni mpya tatu katika uongozi wa ofisi yake.
Kanuni hizo zinalenga pamoja na mambo mengine, katika uimarishaji wa umakini, uadilifu, uwazi na kuhakikisha usawa wa kijinsia kwa watumishi wa ofisi hiyo kuhuku suala la maadili, ufanisi na weledi likitiliwa mkazo.
Wazungumzaji wengi waliopata fursa ya kuchangia majadiliano ya marekebisho ya utendaji kazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, akiwako Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ramadhan Mwinyi, wamesema uhaba waraslimali fedha na raslimali watu ni moja ya mambo yanayochangia utekelezaji hafifu wa majukumu ya Baraza hilo ambalo lina ajenda nyingi kupita uwezo wake.
Wamependekeza kwamba ili utendaji wa Baraza hilo uwe wenye tija, baadhi ya mambo yanayotakiwa kufanyiwa marekebisho ni pamoja na kupunguzwa kwa ajenda na mikutano inayopelekwa kwenye Ofisi ya Rais wa Baraza Kuu. Pamoja na uhakiki wa mtu anayeteuliwa kuwa Rais wa Baraza hilo.
Baadhi ya mapendekezo mengine na ambayo yamepewa umuhimu na wazugumzaji wengi ni pamoja na mchakato wa kumpata Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Mawazo na hoja za wazugumzaji na wachangiaji wengi yamejielekeza katika kutaka mchakato huo uwe wazi, shirikishi na utakaotoa nafasi ya waombaji wengi na ambapo watachujwa baada ya kila mmoja kuhojiwa.
Akizungumzia hoja ya mchakato wa kumpata Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Balozi Ramadhani Mwinyi amesema, Tanzania inaounga mkono hoja ya wanawake kupewa nafasi ya kugombea nafasi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
“ Tanzania inaamini kwamba baada ya miongo miwili ya kutetea na kupigania fursa sawa kwa wanawake na uwezeshwaji wao, tutaweza kushuhudia ushiriki wa wanawake wenye uwezo katika kugombea nafasi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Na hili kwetu sisi itakuwa ni moja ya mafanikio ya maadhimisho ya miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa”. Akasema Balozi Mwinyi umarishaji wa utendaji kati ya Ofisi ya Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Tanzania, Mwakilishi huyo wa Tanzania, amesema, Tanzania inaunga mkono hoja ya uimarishwaji wa ofisi hiyo, uimarishwaji ambao pia utahusishwa utunzaji wa kumbukumbu zote muhimu zinazohusiana na kazi za ofisi ya Rais pamoja na uwepo wa watendaji wenye sifa kutoka mataifa mbali mbali bila ya upendeleo.
Na ili kufanikisha maboresho hayo, kama ilivyokuwa kwa wazungumzaji wengine, Tanzania imesisitiza haja na umuhimu wa kupitia upya bajeti ya Ofisi ya Rais wa Baraza Kuu ili kuhakikisha kuwa inakuwa na bajeti ya kutosha wakati wote.
Na hili kwetu sisi itakuwa ni moja ya mafanikio ya maadhimisho ya miaka 70 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa”. Akasema Balozi Mwinyi umarishaji wa utendaji kati ya Ofisi ya Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Tanzania, Mwakilishi huyo wa Tanzania, amesema, Tanzania inaunga mkono hoja ya uimarishwaji wa ofisi hiyo, uimarishwaji ambao pia utahusishwa utunzaji wa kumbukumbu zote muhimu zinazohusiana na kazi za ofisi ya Rais pamoja na uwepo wa watendaji wenye sifa kutoka mataifa mbali mbali bila ya upendeleo.
Na ili kufanikisha maboresho hayo, kama ilivyokuwa kwa wazungumzaji wengine, Tanzania imesisitiza haja na umuhimu wa kupitia upya bajeti ya Ofisi ya Rais wa Baraza Kuu ili kuhakikisha kuwa inakuwa na bajeti ya kutosha wakati wote.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni