Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (kushoto) akimpokea Rais wa Afrika ya Kusini Mhe. Jacob Zuma (anayeshuka kwenye ngazi), Rais Zuma amewasili nchini kwaajili ya kuudhuria sherehe za uapisho wa Rais Mteule Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli zitakazofanyika hapo kesho katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Rais Zuma akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Mhe. Radhia Msuya (wa kwanza kulia).
Balozi wa Tanzania nchini UAE Mhe. Mbarouk Nassoro Mbarouk (kushoto) akisalimiana na Waziri wa Maendeleo ya Jamii UAE.
Picha na Reginald Philip.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni