Ghasia zimeibuka baada ya mwanaume
mwenye umri wa miaka 42 kutangazwa kuwa mshindi katika shindano la
mtu mwenye sura mbaya Jijini Harare nchini Zimbabwe, huku mashabiki
wakiwatuhumu majaji kwa upendeleo.
Majaji hao walimchagua, Mison Sere,
kuwa mshindi kutokana na kutokuwa na meno mengi na kuwa na uwezo wa
kuibadilisha sura yake kwa kuikunja kunja, na kumshinda bingwa
mtetezi William Masvinu, ambaye amekuwa bingwa tangu mwaka 2012.
Mshindi wa shindano la mwanaume
mwenye sura mbaya nchini Zimbabwe, huibuka na zawadi ya dola 500,
ambayo ni fedha nyingi ukizingatia wengi wa washiriki wa shindano
hilo huwa hawana ajira maalum.
Washiriki wa sura mbaya wakiwa katika mapozi tofauti
Mshindi wa shindano la sura mbaya Mison Sere akiwa amebebwa juu
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni