.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 1 Novemba 2015

UCHUNGUZI WA NDEGE YA URUSI ILIYOANGUKA ENEO LA SINAI MISRI WAANZA

Uchunguzi umeanza baada ya ndege ya Urusi kuanguka eneo la Sinai nchini Misri na kuuwa watu wote 224 waliokuwemo kwende ndege hiyo.

Waziri Mkuu wa Misri amesema hitilafu ya kiufundi huenda ndio chanzo cha ajali hiyo na kukanusha madai kuwa kundi la Dola la Kiislama ndilo lililohusika kuiangusha ndege hiyo.

Hata hivyo makampuni matatu ya ndege ya Emirates, Air France pamoja na Lufthansa yameamua kutorusha ndege zake katika eneo la Sinai hadi hapo taarifa zaidi kuhusiana na tukio hilo zitakapopatikana.

Urusi imetangaza siku moja ya maombolezo kufuatia tukio hilo baya la ajali ya ndege.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni