Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe (katikati chini) akimsubiria Rais wa Zimbabwe Mhe. Robert Mugabe (katikati juu kwenye ngazi) alipokuwa akiteremka kwenye Ndege, Rais Mugabe amewasili nchini kwaajili ya kuhudhuria Sherehe za uapisho wa Rais Mteule Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli zitakazofanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Waziri Membe akimpokea Rais Mugabe (mwenye Ua Mkononi) mara tu baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julias Nyerere jijini Dar es Salaam.
Rais Mugabe akiangalia kikundi cha wapiga Tarumbeta huku Waziri Membe akitoa ufafanuzi wa nyimbi iliyokuwa inachezwa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni