.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 6 Novemba 2015

WANAWAKE WA IRELAND WAMTUMIA SIKU ZAO ZA HEDHI WAZIRI MKUU

Wanawake nchini Ireland wamekuwa wakimtumia ujumbe wa twitta Waziri Mkuu wao Enda Kenny unaoelezea siku zao za hedhi, katika kuonyesha hasira zao dhidi ya sheria kali za kuzuia utoaji mimba.

Mchekeshaji Grainne Maguire ndiye alianza kumtumia ujumbe wa aina hiyo Waziri Mkuu Kenny siku ya jumatatu katika kutaka kuondolewa kifungu cha nane cha mabadiliko ya Katiba ya Ireland.

Mabadiliko ya Katiba ya kifungu hicho yanaruhusu kuokoa maisha ya mama pale tu ujauzito utakapotishia uhai wa mjamzito na ni kosa kisheria kutoa mimba.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni