Wapwa wawili wa mke wa rais Nicolas
Maduro wa Venezuela wamekamatwa Haiti na kupelekwa Marekani
kukabiliana na mashtaka ya usafirishaji wa dawa za kulevya.
Vyombo vya habari vya Marekani
vimewataja ndugu hao wa mke wa rais wa Venezuela kuwa ni Franqui Francisco Flores-de Freitas
na Efrain Antonio Campo-Flores na wanakabiliwa na tuhuma za kushiriki
kuingiza kilo 800 za cocaine Marekani.
Watuhumiwa hao wawili wanatarajiwa
kufika mbele ya mahama ya shirikisho Jijini New York hii leo.
Serikali ya Venezuela haijatoa kauli yoyote kuhusiana na ripoti hiyo
ya kukamatwa kwa ndugu wa mke wa rais.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni