Rais Vladimir Putin wa Urusi
ameagiza uchunguzi kuhusiana na madai ya wanariadha wa nchi hiyo
wamekuwa katika programu ya matumizi ya dawa za kuongeza nguvu.
Bw. Putin ametoa kauli yake hiyo kwa
mara ya kwanza tangu Tume Huru ya Wakala wa Dunia wa Kukabiliana na
Dawa za Kuongeza nguvu Michezoni (WADA) kubainisha tuhuma hizo nzito
jumatatu wiki hii.
Rais Putin amesema kuwa anataka
kuwepo kwa ushirikiano wa kitaalum na vyombo vya kukabiliana na dawa
za kuongeza nguvu kwa wanamichezo. Amesema mashindan ya michezo
yanavutia iwapo hapatakuwa na udanganyifu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni