.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 12 Novemba 2015

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI WA KENYA AONDOA AGIZO LA KUKAMATWA WAANDISHI

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya Joseph Nkaissery ameondoa agizo la kukamatwa waandishi waliochapisha habari zinazohoji jinsi wizara yake ilivyotumia fedha za Kenya shilingi bilioni 3.8.

Licha ya kuondoa agizo hilo jana Waziri Nkaissery ameaendelea kulaumiwa kwa agizo hilo ambalo linakiuka uhuru wa vyombo vya habari kwa mujibu wa Katiba ya Kenya.

Spika wa Bunge Justin Muturi pia alisema kuwa polisi hawana madaraka ya kumkamata mwandishi akiwa eneo la Bunge ambapo ndipo mhariri John Ngirachu alikamatwa bila ya kutolewa agizo la mamlaka ya Spika.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni