.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 19 Novemba 2015

WAZIRI MKUU WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NI MH KASSIM MAJALIWA

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Mh Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungao wa Tanzania. 

Uteuzi huo umetangazwa na Spika wa Bunge, Mh Job Ndugai mbele ya Wabunge mjini Dodoma asubuhi hii kuwa Mh Majaliwa ndiye mteule wa Rais katika nafasi hiyo ya Uwazi Mkuu katika serikali yake ya wamu ya tano

Akilisoma jina hilo baada ya kufungua bahasha iliyokuwa na jina toka kwa Mh Rais, Spika alisema barua hiyo ilikuwa imeandikwa kwa mkono bila kuchapwa, na hata alipolisoma jina la Mh Majaliwa bunge lililipuka kwa shangwe na furaha. 

Ndugu Kassim Majaliwa ni Mbunge wa Ruangwa kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, na pia aliwahi kuwa Naibu Waziri Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa katika ofisi ya Waziri Mkuu wakati wa serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Mstaafu, Mh Jakaya Mrisho Kikwete. 

Jina lake sasa linasubiria kupitishwa na wabunge kwa kupigiwa kura.

Na taarifa kutoka Bungeni mjini Dodoma zinasema kuwa baada ya kura kuhesabiwa, Mh Kassim Majaliwa amepitishwa na Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania baada ya kupata jumla ya kura 258 sawa na asilimia 73.5%

Kura 91 sawa na asilimia 25.9% zilisema hapana na kura 2 ziliharibika.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni