.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 16 Desemba 2015

ABIRIA ZAIDI YA 300 WANUSURIKA KATIKA AJALI YA MELI YA ROYAL ILIYOKUWA INATOKA UNGUJA KWENDA PEMBA

                                                               Sehemu ilishika moto katika meli ya Royal. 
Zaidi ya abiria 300 wamenusurika baada ya moto kuwaka katika chumba cha injini ya meli ya Royal iliyokuwa ikitoka Unguja kwenda Pemba hii leo. 

Taarifa kutoka visiwani Zanzibar zinasema kuwa, baada ya kutokea hitilafu hiyo ya moto, bahati nzuri meli ya Serengeti iliyokuwa inatokea Pemba kwenda Unguja ilipofika eneo la tukio ilitoa msaada ikiwa ni pamoja na kuwahamisha abiria toka meli hiyo ya Royal.  

Taarifa zaidi zinasema kuwa, wakati tukio hilo linatokea, meli hiyo ya Royal ilikuwa na abiria wapatao 374, watu wazima wakiwa ni 300 na watoto 74.
 Abiria wakipatiwa msaada wa kuokolewa kutoka meli ya Royal kuhamishiwa Mv Serengeti
                                                     Meli ya Royal ikivutwa na meli ya Mv Serengeti

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni