Mkuu
wa Mkoa wa Mbeya akifungua semina ya kuwaelimisha na kuwahamasisha
watumiaji wa Huduma za Mawasiliano iliyoandaliwa na Baraza la Ushauri
la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano (TCRA-CCC) katika ukumbi wa Mkapa
jijini Mbeya Desemba 15 -2015 ).Picha Emanuel Madafa
|
Mwenyekiti
Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano
(TCRA-CCC)Ndugu Stanley Mwabulambo (kulia) pamoja na Meneja wa
Mawasiliano TCRA Kanda ya Nyanda za juu kusini Mhandisi Lilian Mwangoka
wakimsikiliza kwa umakini Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro katika
ufunguzi wa semina ya kuwaelimisha na kuhamasisha watumiaji wa huduma za
Mawasiliano Mkoa wa Mbeya Desemba 15 katika ukumbi wa Mkapa jijini
Mbeya.
|
Wananchi
na baadhi ya watumishi wa serikali na mashirika binafsi wakisikiliza
kwa Makini Hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Abbas Kandoro katika
semina ya kuwaelimisha na kuwahamasisha watumiaji wa huduma za
Mawasiliano Mkoa wa Mbeya Desemba 15 mwaka huu katika Ukumbi wa Mkapa
jijini Mbeya.
|
Katibu
Tawala Mkoa wa Mbeya Ndugu Mariam Mtunguja akizungumza katika semina ya
kuwaelimisha na kuhamasisha watumiaji wa wa huduma za Mawasiliano Mkoa
wa Mbeya Desemba 15 Mwaka huu katika Ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya.
|
Mwenyekiti
wa Baraza la Ushauri la watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Ndugu
Stanley Mwabulambo akitoa neo katika semina hiyo ya kuelimisha na
kuhamasisha watumiaji wa Huduma za mawasiliano Mkoa Mbeya Desemba
15-2015 katika ukumbi wa Mkapa jijini mbeya.
|
Wadau wakifuatilia mkutano
|
Kaimu
Katibu mtendaji Baraza la Ushauri watumiaji wa Huduma za Mawasiliano
TCRA-CCC Ndugu Mary Msuya akiwasilisha maada kwa wanasemina juu ya haki
na wajibu wa Mtumiaji wa huduma za Mawasilino katika semina hiyo yenye
lengo la kuelimisha na kuhamsisha watumiaji wa huduma hizo Desemba 15
mwaka huu katika Ukumbi wa Mikutano Mkapa jijini Mbeya.
|
Mhandisi
toka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Kanda ya Nyanda za juu kusini
Mbeya ( TCRA( Asajile Mwakisisile akitoa maada katika semina hiyo.
|
Mmoja wa washiriki katika semina hiyo akichangia katika semina .
|
Mjumbe
wa Baraza la Huduma za Mawasiliano (TCRA-CCC) Ndgugu Nyanda Shuli
akitoa Maada juu ya Muundo ,Kazi na Majukumu ya Baraza la watumiaji wa
Huduma za Mawasiliano katika semina ya kuelimisha na kuhamasisha
watumiaji wa huduma za mawasiliano Mkoa wa Mbeya Desemba 15 mwaka huu
katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mkapa jijini Mbeya.
|
Washiriki wa semina hiyo ya Uhamasishaji na uelimisha wa huduma za Mawasilino wakifuatilia kwa Makini semina hiyo.
|
Picha ya pamoja na Meza Kuu.
|
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro ameyaasa Makampuni ya huduma za Mawasiliano ya Simu Nchini kuhakikisha yanaboresha huduma zao kwa kuhakikisha yanaondoa kero zote anazo kutana nazo mtumiaji wa mawasilino hayo.
Amesema moja ya changamoto inayowakwaza watumaiji wa mawasilino hayo ni pamoja na kuweka matangazo ya simu (Miito ya simu)ambapo hukatwa kiasi cha pesa pasipo makubalino.
Mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Abbas Kandoro ametoa kauli hiyo jijini Mbeya wakati akifungua semina ya kuelimisha na kuhamasisha watumiaji wa huduma za mawasiliano iliyondesha na Baraza la Ushauri la watumiaji wa huduma za mawasilino TCRA-CCC katika ukumbi wa Mkapa jijini humo.
Amesema pamoja na kutambua mchango wa makampuni yanayotoa huduma hizo za mawasiliano katika kuleta maendeleo ,nivyema makampuni hayo yakahakikisha yanatoa huduma zenye ubora wa hali ya juu unaonekana na thamani inayolipwa na watumiaji wa huduma hizo sanjali na kutimiza majukumu yao kwa watumiaji kama yalivyo ainishwa katika sheria na kanuni za leseni.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa wa Mbeya amewataka watumiaji huduma hizo za mawasiliano ya simu kujikita katika matumizi bora ya mitandao ya simu badala ya kujingiza katika matumizi yasiyo sahihi ambayo yamekuwa yakichangia kwa kiwango kikubwa kuondoa maadili katika jamii pamoja na uchochezi.Amesema kuwa sheria ya makosa ya mitandao nchini namba 14 inaweka wazi juu ya adhabu atakayo weza kutolewa dhidi ya mtu au kikundi kitakacho husika na upotoshwaji wa aina yoyote .
Amesema sheria ya makosa ya mitandao inaanisha makosa na adhabu zinazohusiana na matumizi ya mfumo wa kompyuta na teknolojia ya habari na mawasilino.
Hata hivyo Mkuu huyo wa mkoa wa mbeya ametumia fursa hiyo kulitaka baraza la ushauri la watumiaji wa huduma za mawasiliano TCRA- TCCC kuendelea kuhamasisha ,kuelimisha pamoja na kutambua na kuelewa kero na matalajio ya watumiaji wa huduma za mawasiliano nchi.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la watumiaji wa huduma za mawasiliano Ndugu Stanley Mwabulambo ametoa wito kwa Makampuni yote yaliyojikita katika uwekezaji wa mawasiliano ya simu ,huduma za utangazaji na huduma za posta kuhakikisha wanaendelea kujenga mitandao ya huduma zao nchi nzima ili kuwawezesha wananchi kushiriki katika maendeleo.
Aidha Mwenyekiti huyo ameviomba vyombo vya habari nchini kusaidia kulitangaza Baraza hilo na shughuli zake ili wananchi wajue ni wapi pa kupata ushauri na kutatua matatizo yao yanayohusiana na huduma za mawasiliano.Katika semina hiyo pamoja na kutoa elimu kwa watumiaji Baraza pia limeunda kamati ya watumiaji wa huduma za mawasililiano kwa mkoa wa mbeya ambapo wajumbe wa kamati hiyo walichaguliwa kutoka miongoni mwa wanasemina ambapo majukumu yao yatakuwa ni kuelimishajamii juu ya haki wajibu na utaratibu wa kuwasilisha malalamiko sanjali na kupokea toka kwa watumiaji na kuyawasilisha kwa baraza.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni