Mamlaka za Jiji la Beijing nchini
China zimetoa tahadhari ya pili ya uchafuzi wa hewa, ikiwa ni chini
ya wiki tangu itoe tahadhari kama hiyo kwa mara ya kwanza.
Jiji hilo kuu la China litakuwa na
moshi mzito kuanzia jumamosi hadi jumanne, Idara ya Hali ya Hewa ya
Beijing imeeleza.
Kituo cha Mamlaka ya Hali ya Hewa
cha Taifa China, kimesma maeneo ya Xian kati kati ya China na Harbin
kaskazini mashariki nayo yataathiriwa na hali ya hewa ya moshi.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni