Papa Francis ameridhia kutambua
muujiza wa pili uliofanywa na Mama Teresa, na kufungua milango kwa
mtawa huyo wa Kanisa Katoliki kutangazwa mtakatifu mwakani.
Muujiza huo unahusiana na Mama
Theresa kumponya mwanaume mmoja wa Brazil aliyekuwa na uvimbe kwenye
ubongo mwaka 2008, Vatican imesema.
Mama Teresa alikufa mwaka 1997, na
aliingizwa katika mchakato wa kutangazwa mtakatifu mwaka 2003.
Mtawa huyo ameshinda Tuzo ya Nobeli
kwa kazi zake kwa masikini wa makazi duni katika mji wa Calcutta
nchini India.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni