.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 15 Desemba 2015

JAHAZI LA CHELSEA LAZIDI KUTOTA, HUKU MOURINHO AKIHISI KUHUJUMIWA

Mshambuli wa Leicester City Jamie Vardy na Riyad Mahrez wameisaidia timu yao kurejea kileleni mwa ligi kuu ya Uingereza na kuisukuma chini zaidi ya msimamo wa ligi timu ya Chelsea.

Katika mchezo huo ambao Chelsea ilikuwa ugenini ilijikuta ikifungwa bao la kwanza na Jamie Vardy katika dakika ya 34, kabla ya Riyad Mahrez kupachika la pili dakika ya 48, huku Loic Lemy akiipatia Chelsea bao pekee la kufutia machozi.

Baada ya kipigo hicho cha mabao 2-1 kocha wa Chelsea Jose Mourinho amesema anajihisi kama kazi yake inahujumiwa, huku akishuhudia akipoteza mchezo wa tisa kati ya michezo 16 ya Ligi Kuu ya Uingereza.
                                   Jamie Vaedy akipachika bao la kwanza kwa Leicester City
                 Benchi la ufundi la Chelsea likiwa hoi pamoja na wachezaji wa akiba

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni