Gareth Bale ametikisa nyavu mara nne
wakati Real Madrid ikifanya maafa makubwa ya funga mwaka kwa Rayo
Vallecano kwa kuichakaza kwa magoli 10-2 katika Ligi ya La Liga.
Katika mchezo huo Real ili kuwa
nyuma kabla ya mchezaji wa Vallecano Tito kutolewa kwa kadi nyekundu,
licha ya Danilo kuifungia goli la kwanza kabla ya Antonio Amaya na
Jozabed.
Bale alisawazisha kwa goli la kichwa
kabla ya Raul Baena kutolewa nje kwa kadi nyekundu na Cristiano
Ronaldo kufunga kwa mkwaju wa penati.
Baadae Bale akaongeza mabao matatu
zaidi, Ronaldo akafunga lapili na Karim Benzema kufunga mabao matatu
yaani hat-trick na idadi ya mabao kuwa 10-2.
Katika matokeo mengine Málaga 1 - 0
Atl Madrid, Ath Bilbao 2 - 0 Levante, Granada CF 0 - 2 Celta de Vigo
na Real Sociedad 0 - 2 Villarreal.
Gareth Bale akishangilia baada ya kucheka na nyavu
Cristiano Ronaldo akiwa juu angani kupiga mpira kwa kichwa na kufunga bao



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni