Samaki na Mafuta ya samaki ambayo ni muhimu katika mwili
|
Brokali
|
Nyanya
#AfyaYako Vyakula Vinavyoongoza kuongeza AKILI kwenye ubongo
Ifuatayo ni orodha ya vyakula ambavyo vinaongoza kwa kuimarisha utendaji kazi mzuri wa ubongo:
1.MAFUTA YA SAMAKI
Mafuta
ya samaki ni muhimu kwa ubongo na mfumo wa ufahamu. Ulaji wa samaki
wenye minofu kama samoni (salmon) na dagaa, utaweza kupata faida hizo
kwa sababu aina hii ya samaki ina kiasi kingi cha mafuta ya Omega 3
ambayo huimarisha utendaji kazi na mawasiliano kati ya ubongo na seli za
mwili moja kwa moja.
2.PILIPILI KALI
Pilipili
kali nayo huwa ni chakula kikubwa cha ubongo kwa sababu ina kiwango
kingi cha Vitamin C ambayo huhitajika zaidi kwenye ubongo, pilipili
inaaminika kuwa na kiwango kingi cha vitamin hiyo kuliko hata machungwa.
3.MBEGU ZA MABOGA
Mbegu
za maboga zina kiwango kingi cha madini ya ‘Zinc’ ambayo husadia
kuongeza kumbukumbu (memory). Kuna njia nyingi za kula mbegu za maboga,
moja wapo ni kuzikaanga na kula kama karanga, ukila kiasi cha kiganja
kimoja kwa siku, inakuwa poa.
4.NYANYA
Nyanya
ni muhimu sana kwa sababu huzuia magonjwa ya ubongo (brain disease)
kutokana na kuwa na kirutubisho aina ya ‘Lycopene’ chenye uwezo wa
kuzuia magonjwa nyemelezi yanayoweza kutokea. Hivyo ulaji wa nyanya
utakusaidia kukupa kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali, yakiwemo ya
akili.
5. BROKOLI
Brokoli
ni mboga ya majani aina fulani kama maua ya maboga, ambayo nayo
inafaida sana kwenye ubongo, ina vitamin K, C na inatoa kinga ya mwili.
Vitamin K inahusika moja kwa moja na utendaji kazi mzuri wa ubongo na
husaidia kuzuia magonjwa yatokanayo na uzee.
6.KARANGA
Aina
zote za karanga zina vitamin E, ambayo huzuia tatizo la upotevu wa
kumbukumbu na pia zina mafuta yenye afya yanayohitajika mwilini.
7.MAYAI
Mwisho
ni mayai ya kuku, ambayo yana kirutubisho aina ya Choline. Kirutubisho
hiki huzalishwa mwilini kwa kiwango kidogo tu, hivyo kwa kula mayai (ya
kienyeji) utaweza kuongeza kiwango cha kirutubisho hicho mwilini kwa
kiwango kikubwa na hivyo kuimarisha afya ya ubongo.
CHANZO CRI SWAHILI
|




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni