Kiongozi wa jamii ya Lango nchini
Uganda Dk. Michael Odongo Okune amewaonya wanawake wa kabila la Langi
kuhusiana na tabia ya kuwapiga wanaume wao kutokana na vitendo hivyo
kuongezeka mno.
Akiongea na waombolezaji kwenye
maziko ya Rose Omona Odyebo wilyani Oyam, Dk. Odongo amesema viongozi
wa kimila wa Lango hawatovumilia ukatili na vipigo katika ngazi ya
familia vinavyofanywa na wanawake ama wanaume.
Dk. Michael Odongo Okune ambaye pia
ni Waziri wa Kimila wa Lango ameonyesha kukerwa na vitendo vya
wanawake wa kabila la Langi kuwadunda wanaume zao, hali inayochochea
vurugu kwenye familia.


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni