.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 23 Januari 2016

ABIRIA 2 WAMEFARIKI DUNIA NA WENGINE 36 WAMEJERUHIWA KUFUATIA AJALI YA BASI LA BM

                                                                           Basi la BM baada ya kupata ajali. 
Abiria 2 wamefariki dunia na wengine 36 wamejeruhiwa kufuatia ajali ya basi la BM lenye namba za usajili T 619 BQX lililokuwa linatoka jijini Dar es Salaam kwenda Morogorogo kupinduka jana usiku. 

Mashuhuda wamesema kuwa, ajali hiyo ilitokea katika eneo la Lubungo - Mikese katika barabara kuu ya Morogoro - Dar es Salaam jana saa tatu na nusu usiku. 

Chanzo cha ajali hiyo inaelezewa kuwa ni mwendo kasi wa dereva la basi hilo, ambapo aligonga lori lililokuwa linakuja mbele yake hivyo kusababisha basi hilo kupinduka zaidi ya mara mbili upande wa pili wa barabara ambako kuna bonde. Majeruhi walikimbizwa hospitali ya mkoa wa Morogoro kwa matibabu.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni