Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akizungumza na raia wa China wanaoishi nchini, katika sherehe yao ya kuukaribisha mwaka mpya iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake, Waziri Kitwanga alisema Tanzania inatambua ushirikiano mzuri wa miaka mingi uliopo kati yake na China, hivyo raia yeyote wa kigeni anatakiwa afuate taratibu za kuishi nchini, na operesheni inayoendelea ya kuwakamata raia wa kigeni, kamwe haitagusa wenye vibali halali. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kikundi cha Karate kinachoongozwa na raia wa China wanaoishi nchini kikitoa burudani katika sherehe yao ya kuukaribisha mwaka mpya iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, jijini Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (hayupo pichani) ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hiyo, katika hotuba yake alisema nchi yake inatambua ushirikiano mzuri wa miaka mingi uliopo kati yake na China, hivyo raia yeyote wa kigeni anatakiwa afuate taratibu za kuishi nchini, na operesheni inayoendelea ya kuwakamata raia wa kigeni, kamwe haitagusa wenye vibali halali. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Sehemu ya raia wa China wanaoishi nchini, wakimsikiliza kwa makini, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (hayupo pichani) wakati alipokuwa anatoa hotuba yake kwa Wachina hao katika sherehe yao ya kuukaribisha mwaka mpya iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, jijini Dar es Salaam jana. Waziri Kitwanga katika hotuba yake alisema nchi yake inatambua ushirikiano mzuri wa miaka mingi uliopo kati yake na China, hivyo raia yeyote wa kigeni anatakiwa afuate taratibu za kuishi nchini, na operesheni inayoendelea ya kuwakamata raia wa kigeni, kamwe haitagusa wenye vibali halali. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI,
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni