Nafasi ya Arsenal ya kuongoza
msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza kwa tofauti ya pointi, iliota mbawa
jana baada ya Joe Allen kuisawazishia Liverpool na kuipatia pointi
moja muhimu kwenye dimba la Anfield.
Katika mchezo huo ulioishia kwa sare
ya mabao 3-3 Oliver Giroud alipachika wavuni mabao 2 na kukosa moja
la wazi na kufanya idadi ya mabao aliyofunga katika msimu huu kufikia
18, wakati Arsenal ikiwa inaongoza kwa mabao 3-2 kabla ya Liverpool
kusawazisha dakika ya 90.
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger akiduwaa baada ya koporwa ushindi dakika za mwisho.
Soka sio lelemama Diego Costa na McAULEY wakianguka chini
Katika mchezo mwingine bao la
kusawazisha katika dakika za mwisho la James McClean, limeipora
ushindi Chelesea na kuipatia pointi moja West Brom katika mchezo
ulioishia kwa sare ya mabao 2-2 katika dimba la Stamford Bridge.
Refa akimzuia Diego Costa asipigane na Olsson
Matokeo mengine ya mechi za Ligi Kuu
ya Uingereza jana Man City 0 - 0 Everton, Southampton 2 - 0
Watford, Stoke 3 - 1 Norwich, Swansea 2 - 4 Sunderland na Tottenham 0
- 1 Leicester.




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni