Bondia Danny Garcia amemdunda kwa
pointi Robert Guerrero na kuweka mazingira ya kupata mchezo wa
marudiano na Amir Khan.
Garcia aliyeanza vibaya alibadilika
taratibu na kuweza kuzimudu vyema raundi zilizofuatia baadae na
kufanikiwa kushinda mkanda wa uzito wa welterweight WBC.
Garcia ameweza kushinda mchezo huo
ulioshuhudiwa na Khan aliyemtwanga kwa KO mwaka 2012, pia alikuwapo
Floyd Mayweather akitazama pambano hilo la mkanda huo ambao aliwahi
kuutwaa.
Bondia Robert Guerrero akimtwanga ngumi ya kushoto Danny Garcia
Danny Garcia akimpa konde la chini ya kwapa Guerrero
Floyd Mayweather akiwa na Mchekeshaji Dave Chappelle wakifuatilia pambano hilo




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni