Theluji kubwa iliyofunika mashariki
mwa Marekani imewafanya wakazi wa majiji ya New York na Washington DC
wanaofikia milioni 85 kukwama kufanya shughuli zao za kila siku.
Theluji hiyo inafikia upana na
sentimita 102 katika baadhi ya maeneo, imefanya huduma za usafiri wa
reli na ndege kukwama, huku umeme ukikatika kwa watu wapatao 200,000.
Amri ya kutosafiri iliyowekwa Jijini
New York lililoshuhudia theluji kubwa iliyoshuka na kuweka rekodi,
inatarajiwa kuondolewa baadae leo.
Mtu akikatiza kati kati ya magari yaliyofunikwa na theluji nchini Marekani
Wanajeshi wakijaribu kuondoa theluji baada ya gari lao kukwama
Mtu akitumia mbwa kumvuta kwenye theluji




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni