Bunge la nchini Denmark litapigia
kura pendekezo lenye utata mkubwa la kushikilia mali zenye thamani za
wahamiaji wanaoomba hifadhi ili kufidia kulipia gharama za kuwatuza.
Pendekezo hilo linakabiliwa na
ukosoaji mkubwa nchini humo pamoja na nje ya nchi hiyo tangu
lilipotangazwa na serikali ya Denmark mapema mwezi huu.
Mamlaka za nchi hiyo zimesisitiza
kuwa sera hiyo inawafanywa wahamiaji wawe sawa na raia wa Denmark
wasio na ajira, ambao hulazimishwa kuuza vitu vyao vya thamani vya
kiasi fulani ili kunufaika na msaada wa serikali.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni