Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira
wa Miguu nchini (TFF), Mwesigwa Selestine leo amefungua kozi ya ngazi
ya juu ya ukocha kwa wanawake (High Level Coaching Course)
iliyoandaliwa na TFF kwa kushirikiana na FIFA.
Akiongea na waandishi wa habari
wakati wa ufunguzi wa kozi hiyo, Mwesigwa amewataka washiriki wa kozi
hiyo kuzingatia mafunzo hayo na kuitumia vyema fursa hiyo adimu
waliyoipata.
Mwesigwa amewataka washiriki
kuhakikisha kozi hiyo ya siku tano, inawasaidia na kwenda kuwa walimu
wa mpira wa miguu kwa wanawake, na kuongeza mwamko kwa wanawake wengi
kuupenda na kuucheza mpira wa miguu.
Aidha Mwesigwa, amewataka washiriki
wa kozi hiyo kuzingatia maelekezo ya mkufunzi, nidhamu ya ndani na
nje ya uwanja kwani imekua ni bahati nzuri kwao kupata nafasi ya
kushiriki kozi hiyo ya ngazi ya juu.
Naye mkufunzi wa kozi hiyo
anayetambulika na FIFA/CAF, Sunday Kayuni amesema atatumia uwezo wake
wote kuhakikisha washiriki wa kozi hiyo wanajifunza na kuelewa vizuri
mafunzo yake, ili waweze kuwa walimu wazuri watakapokwenda kuanza
kufundisha.
Mwenyekiti wa Kamati ya Soka la
Wanawake ya TFF, Amina Karuma ameishukuru TFF kwa kuendesha kozi hiyo
na kusema kupatikana waalimu wengi wa kike kutaongeza mwamko wa
wanawake kuucheza mpira wa miguu.
Jumla ya washiriki 25 wanashiriki
kozi hiyo kutoka mikoa mbalimbali nchini ambao ni Fatuma Omary,
Esther Chabruma, AMina Mwinchum, Sweetie Charles, Pendo John, Berlina
Mwaipungu, Mariam Mchaina, Elizabeth Sokoni, Sophia Mkumba, Marry
Masatu, Aziza Mbwele, Fadhila Yusuph.
Wengine ni Veneranda Mbano, Mariam
Aziz, Hilda Masanche, Chichi Mwidege, Sophia Edward, Asha Rashid,
Fatuma Khatibu, Neema Sanga, Hindu Muharami, Tatu Malogo, Komba
Alfred, Veroinca Ngonyani, Judith nyatto na Ingfridy Kimaro.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni